HIVI NDIVYO UKAME ULIVYOIKUMBA AFRIKA KUSINI, SERIKALI YASEMA NI JANGA LA KITAIFA.

Afrika Kusini imetangaza ukame unaoikumba nchi hiyo kuwa janga la kitaifa kutokana na hali mbaya inayoikumba nchi hiyo baada ya mvua kukosa kunyesha ipasavyo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.
Taarifa zinasema serikali imetathmini hali ya mambo na kubaini kubwa nchi hiyo inakumbwa na tatizo kubwa sana.
Hayo yanaripotiwa wakati mji wa Cape Town wa Afrika Kusini umezindua kituo cha kukabiliana na maafa DOC ili kujiandaa kukabiliana na hali mbaya kabisa iliyosababishwa na ukosefu wa maji katika mji huo muhimu wa bandari.
Habari zinasema maji ya bomba yatakatwa kama kina cha maji kwenye mabwawa kitafika kiwango cha asilimia 13.5. Kwa sasa kiwango cha maji kwenye mabwawa kimefikia asilimia 26.7, na kama hali itaendelea kama ilivyo kiwango cha maji kitafikia asilimia 13.5 ifikapo Juni 11.
Ukame umekumba maeneo makubwa ya kusini na magharibi mwa Afrika Kusini na pia nchi kadhaa za eneo zima la kusini mwa Afrika.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani (WFP) limetahadharisha kuhusu kuenea njaa eneo la kusini mwa Afrika. 
Taarifa hiyo ya WFP imesema uhaba wa mvua na viwavi jeshi wanaoharibu mimea ya mazao ndiyo sababu itakayolitumbukiza eneo la kusini mwa Afrika katika maafa ya njaa huku mamilioni ya watu hasa watoto wadogo wakiwa hatarini.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni