WAJUMBE WA DCC WAIKATAA TAARIFA YA HALMASHAURI, MSALALA.

Image result for kahama map
WAJUMBE wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) Wilayani hapa Mkoani Shinyanga wameiponda taarifa ya utekelezaji ya miradi ya Halmashuri ya Msalala kutokana na kutoonesha vipaumbele vyake waliojiwekea katika kuvitekeleza katika mwaka wa fedha wa 2018/19.

Hali hiyo imekuja baada ya wajumbe  wa kamati hiyo ambayo ilijumuisha kutoka halmashauri tatu ya Ushetu,Mji pamoja na Msalala kutoridhishwa na taarifa hiyo iliyowasilishwa na kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Mshaka Mabula ambaye alisema kuwa hakuwa na taarifa yeyote juu ya kikao hicho na kuongeza taarifa za kikao hicho amezipata asubuhi kabla ya kuanza kwake.

Diwani wa kata ya Ikinda Matrida Msoma ambae pia alikuwa mjumbe wa kikao hicho alisema kuwa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wake hakuonesha mapitio ya mwaka wafedha wa 2017/18 pamoja na mpango wa makisio ya mwaka huo hali ambayo taarifa yetu imeonekana taarifa mbaya kwa wajumbe huku wakiipongeza Halmashauri ua ushetu kwa taarifa nzuri iliyoandaliwa.

Alisema kuwa halmashauri ya Msalala imekuwa ikifanyavema katika miradi ya maendeleo kwa kila kata na kuongeza kama kaimu mkurungenzi angepata taarifa mapema juu ya uwepo katika kikao hichi angefanya vema katika kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuri za miradi ya maendelo ya mwaka 2017/18/2018/19.

Nae diwani wa kata ya Nyankende Doa Limbu alisema kuwa makosa hayo yaliyojitokeza katika Halmashauri ya Msalala katika kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ni jambo la kujifunza kwa halamshauri nyingine ili jambo hili lisiweze kujirudi tena katika vikao vijazo.

Huku diwani wa kata ya Nyihongo katika Halmashauri ya mji Shedrack Mgwami akisema kuwa watalamu wa halamshauri wanapoandika taarifa zao kabla ya kuziwasilisha katika vikao wahakikishe wanashirikisha madiwani hali ambayo itasaidia kuwasilisha taarifa kwa usahihi kama walivyofanya halamshauri ya Ushetu na Mji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mashaka Mabula alikiri kuwepo na mapungufu katika taarifa hiyo nakudai kuwa taarifa juu ya kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya alizipata muda mfupi kabla ya kufika katika kikao hali iliyopelekea kuandaa taarifa hiyo kwa haraka kwa kuhofia angekuta kikao kimeanza.

Aliomba radhi kwa wajumbe wa kikao hicho kutokana na kulalamikiwa kwa taarifa iliyokosa vipengele muhimu hali ambayo taarifa haikujadiliwa kwa muda mrefu kama ilivyo taarifa nyingine za mji na ushetu nakudai kwa kikao kijacho atajitahidi kutimiza yote yanayohitaji kuwepo katika taarifa ili wajumbe wapate la kuchangia.

Aidha Mwenyekiti wa kikao hicho ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu alisema kuwa Halmashauri ya Msalala wamekuwa wakisumbua katika utoaji wa taarifa hata katika Vikao vya kamati ya ulinzi na usalama vya wilaya na kuongeza kuwa hivi karibu moja ya wakuu wa idara alikaimu nafasi ya mkurugenzi alitoa taarifa ambayo wajumbe wa kamti hiyo hawakuridhika nayo.

Na Ally Lityawi,           Kahama.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni