UDOMASA KUANZA MGOMO WA KUTOFANYA KAZI, KAMA MALIPO HAYATOFANYIKA.
Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imeadhimia kufanya kikao cha mwisho tarehe 26 machi mwaka huu chenye lengo la kutofanya kazi kama malipo ya madeni ya watumishi wa umma hayatolipwa.
Kauli hiyo imetolewa chuoni hapo na mwenyekiti wa UDOMASA Shukuru Mlwafu wakati wa kikao cha Wajumbe wa jumuiya hiyo walipokuwa wakijadili nini
kifanyike ili waweze kulipwa madeni yao.
Akifafanua zaidi amesema Jumuiya imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli kuhusu malipo ya watumishi wa umma.
Aidha amesema baada ya mishahara ya wanataaluma wa vyuo vikuu kupitia waraka wa msajili wa hazina wafanyakazi wanataaluma zaidi ya 517 waliahidiwa kulipwa malimbikizo ya mishahara katika mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo mpaka mwaka huo wa fedha ulimalizika bila hata mwanataaluma mmoja kulipwa.
Mlwafu amesema baada ya tamko la Rais Magufuli kutenga Bilioni 200 ikiwa ni pamoja na kulipa madai ya wafanyakazi katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa,
hakuna hata mwanataaluma mmoja kati ya hao 517 aliye katika orodha kwa ajili ya malipo kutokana na pesa hizo.
Katika hatua nyingine wanataaluma hao wameomba wizara zote zinazohusika na madai ya watumishi wa umma zitekeleze agizo la Rais Magufuli kama alivyowaahidi watumishi wa umma, Orodha ya madai ya wafanyakazi ijumuishe wafanyakazi wote wanaidai serikali na kuondokana na kutoa majina machache kama ilivyofanyika sasa na kusababisha taharuki zisizokuwa na ulazima.
Pia, madai hayo yafanyiwe kazi mapema kwa kadiri ya maelekezo ya Rais magufuli pasipokuathiri haki za wafanyakazi ambao mpaka sasa wanatekeleza
wajibu wao.
0 Comments:
Chapisha Maoni