FISI WAZUKA TENA MITAANI KAHAMA, WATEMBEA KWA MAFUNGU.


Baadhi ya wananchi wa kata ya Iyenze Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wamesema bado wana hofu kubwa juu ya maisha yao kutokana na  fisi kuendelea kutembea kwa makundi usika na machana.

Wananachi hao wamesema Fisi hao wamekuwa wakila mifugo na wameiomba serikali iwasaidie kuwadhibiti ili wasiendelee kuleta madhara.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Holohondo, MATHIAS MAILA amesema wamekwisha lifikisha suala hilo katika Halmashauri ya Ushetu ambapo kwa mujibu wa diwani wa kata ya Iyenze, LUCAS MAKURUMO kuanzia Disemba  mwaka jana hadi sasa jumla ya mifugo 52 imeliwa na fisi hao.


Akizungumzia tatizo hilo , Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, NGUSA MAZIKU amesema  baada ya kupata taarifa wamekuwa wakifuatilia mara kwa mara  na  kwamba jamii waendelee kutoa  ushirikiano kwa maafisa maliasili ili kukabiliana na tataizo hilo.


Maeneo mengi ya wilaya ya Kahama hukabiliwa na idadi kubwa ya fisi wanaozagaa katika makazi ya watu na kushambulia mifugo na hata binadamu ambapo hivi karibuni fisi mmoja aliuawa mjini Kahama baada ya kuingia katika uzio wa Hospitali ya wilaya ya Kahama

Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni