WATU 30 WAUAWA KATIKA MAPIGANO YA WENYEWE KWA WENYEWE CONGO

Image result for mapigano congo
Kutokana na mauwaji ya zaidi ya watu 30 yaliyoshuhudiwa huko Ituri kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki;na kusababisha maandamano makali yaliyopelekea vifo vya ziada kwa raia mpema wiki hii.

Gavana wa mkoa Bwana Bwana Penengapa Abdallah Jefferson ametoa mwito kwa makabila yote hasimu;kuwa na umoja badala ya chuki na mzozo wa kikabila.

Licha ya juhudi zinazo endeshwa na wakuu viongozi wa serkali kuhakikisha kwamba amani na usalama vinashuhudiwa kwenye adhi mzima ya nchi hiyo kulitokea mauwaji iliyo na sura ya mzozo wa kikabila mkoani Ituri.

Hali iliyotokea kwenye eneo la wilaya ya Djugu mwishoni mwa wiki raia 34 waliuwawa maeneo ya Blukwa na pembezoni mwa kijiji hicho huku raia kumi na mbili walijeruhiwa na kulazwa kwenye hospitali kuu ya Drodro, mifugo kuteketezwa, na maelefu ya wananchi kuyahama makazi yao kwa ajili ya kunusurisha maisha yao.

Kabila la Wahema likiwatuhumu kabila la Walendo kuwatendea uwalifu huo bila kutoa sababu na chanzo cha uhalifu huo kutokea.

Hata hivyo; Kupitia tangazo liililo sahiniwa na kiongozi wa jamii ya kabila la Wahema Bwana Hadji Ibrahim Ruhigwa Bamaraki na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii;kupinga mauwaji ya watu;kuuwawa kwa mifugo;na takriban nyumba kati ya 1000 na 2000 kuchomwa, na wimbi kubwa la wakimbizi kuyahama makazi yao.

Mwito ulitolewa kwa wakazi wote wenye asili ya kabila lao;kufanya siku mbili bila shughuli zozote,kuanzia jumatatu na jumanne wiki hii;lakini siku ya kwanza ya mgomo;kukashuhudiwa maandamano makali yaliyo pelekea Gavana wa mkoa kurushiwa mawe.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni