Baada ya wiki saba madarakani kocha wa Hamburg SV Bernd Hollerbach aachia ngazi, safari ya kigogo hicho cha soka nchini Ujerumani kuelekea daraja la pili nyeupee ..
Ni timu ambayo haijashuka daraja tangu Bundesliga kuanzishwa mwaka 1963.
Imekwisha kuwa bingwa wa ligi ya taifa Bundesliga mara 6, kombe la shirikisho DFB Pokal mara 3, kombe la washindi barani Ulaya, hivi sasa Europa League mara 1 na Kombe la Ulaya , hivi sasa Champions League mara 1.
Timu hii ni Hamburger SV ambayo kwa jina la utani inaitwa Dino, ama Dinosaurus, wanyama waliokuwa wakiishi katika dunia miaka milioni kadhaa iliyopita ambao sasa hawako tena.
Misimu minne iliypopita Hamburg SV imebadilisha makocha zaidi ya kumi na hakuna hata mmoja aliyeonesha kuiletea uhai timu hiyo licha ya kuiokoa tu dhidi ya kushuka daraja.
Lakini msimu huu hali inaonekana kuwa ngumu zaidi kwani Kocha Bernd Hollerbach aliyeteuliwa kuiokoa timu hiyo naye kibarua kimeota majani.
Hiyo ndio historia fupi ya Hamburg SV ambayo ni ya mafanikio makubwa katika soka la Ujerumani, timu ambayo aliichezea pia mchezaji maafuru wa Ujerumani Kaiza Franz Beckenbauear na mchezaji maarufu wa Uingereza Kevin Keegan.
Lakini hivi sasa imo katika hatari ya kushuka daraja la pili na kumekuwa na mtafaruku mkubwa katika timu hiyo.
Hatua ya kumuondoa Hollerbach imekuja baada ya kichapo cha mabo 6-0 dhidi ya mabingwa watarajiwa FC Bayern.
Mchezaji wa Hamburg SV Sven Schipplock alisema kocha wa vijana wa umri chini ya miaka 21 wa klabu hiyo Christian Titz anatarajiwa kutajwa rasmi kuwa kocha wa timu ya kwanza.
0 Comments:
Chapisha Maoni