LICHA YA UJANGILI KUSHIKA KASI, HALI YA ONGEZEKO LA WANYAMAPORI INARIDHISHA MSUMBIJI

Image result for mozambique national parks
Mamlaka ya hifadhi ya wanyamapori nchini Msumbiji imefafanua kuwa licha ya kiwango cha kutisha cha ujangili, nchi hiyo imekuwa ikisajili matokeo mazuri ya kurejesha wanyama katika hifadhi zake.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo bwana Mateus Muthemba amesema, kuna maendeleo katika baadhi ya maeneo ya hifadhi za taifa kama hifadhi ya Gorongosa.

Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka kumi ya kuwarejesha, mamlaka imefanikiwa kuongeza idadi ya wanyama mara kumi, ambayo inawezesha hifadhi ya wanyama kushirikiana na hifadhi nyingine kote nchini humo.

Hata hivyo mamlaka hiyo imekiri kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kwasababu ongezeko la idadi ya wanyama kwenye hifadhi linaweza kuzuiwa kama vita dhidi ya majangili itashindwa.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni