
Rais Trump wa Marekani amerudia madai yake kwamba Umoja wa Ulaya usitishe vizuwizi vyake vya biashara kwa biadhaa za Marekani ili kunusuru washirika wake hao na ushuru mpya wa chuma cha pua na bati.
Rais wa Marekani amesema hayo baada ya mazungumzo magumu mjini Brussels kati ya wajumbe wa majadiliano wa Umoja wa Ulaya na mwakilishi wa masuala ya biashara wa Marekani Robert Lighthizer katika juhudi za kumaliza mzozo mkubwa ambao wengi wanahofia unaweza kuingia katika vita vikubwa vya kibiashara.
"Umoja wa Ulaya , mataifa safi kabisa ambayo yanaitendea Marekani vibaya kabisa katika biashara, yanalalamika juu ya kodi katika chuma cha pua na bati," Trump alisema.Afisa wa ngazi ya juu wa biashara wa Umoja wa Ulaya amesema Marekani imeshindwa kueleza kwa uwazi juu ya vipi Ulaya na Japan zinaweza kuepuka kodi hizo zinazotarajiwa kuanza wiki ijayo.
"Iwapo wataondoa vizuwizi vyao vibaya kabisa na kodi katika biadhaa za Marekani zinazotozwa hivi sasa, tutafanya hivyo hivyo kuondoa vyetu. Nakisi kubwa. Iwapo hawatafanya hivyo, tutaweka kodi kwa magari. Haki!"
Tangazo la rais Donald Trump la kuweka ushuru wa asilimia 25 kwa chuma cha pua kitakachoingizwa nchini humo na asilimia 10 katika madini ya bati limeuchoma Umoja wa Ulaya, pamoja na washirika wengine wakubwa ikiwa ni pamoja na Japan, ambayo waziri wake wa uchumi Hiroshige Seko pia alihudhuria mazungumzo hayo mjini Brussels.
0 Comments:
Chapisha Maoni