UCHUMI WA RWANDA WAKUA KWA ASILIMIA HIZI......

Related image

Takwimu rasmi zilizotolewa jana na serikali ya Rwanda zinaonyesha kuwa mwaka jana uchumi wa Rwanda ulikua kwa asilimia 6.1, ambayo ni zaidi ya makadirio ya asilimia 5.2.

Idara ya takwimu ya Rwanda NISR imesema sekta ya kilimo imechangia asilimia 31 ya ongezeko la uchumi, huku sekta ya viwanda ikichangia asilimia 16, na sekta ya huduma asilimia 46.

Takwimu pia zimeonyesha kuwa pato la taifa la Rwanda katika mwaka 2017 lilikadiriwa kufikia dola bilioni 9 za kimarekani. 

Katika kipindi cha robo ya nne cha mwaka jana, pato hilo limeongezeka kwa asilimia 10.5.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni