
Klabu ya soka ya Simba imetangaza kikosi kitakachoondoka leo kuelekea Misri kwaajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.
Mkuu wa idara ya habari ya klabu hiyo, Haji Manara amewataja viongozi 7 ambao wataongozana na timu kuwa ni Kocha mkuu Pierre Lichantre, kocha msaidizi Masoud Juma kocha wa viungo Muharam Mohammed na Mohammed Aymen.
Wengine ni daktari wa timu Dr. Yassin Gembe, meneja wa timu Richard Robert na Yassin Mtambo ambaye ni mtunza vifaa. Mchezo huo utapigwa jumamosi Machi 17 huko jijini Port Said Misri.
Wachezaji ni James Kotei, Yusufu Mlipili, Emanuel Okwi, Laudit Mavugo, Shomari Kapombe, Said Hamisi, Mohamed Hussein, Asante Kwasi na Erasto Nyoni. Wengine ni Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, John Bocco, Paul Bukaba, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya, Nicholas Gyan, Said Mohamed 'Nduda', Aishi Manula, Juuko Murushid na Juma Luizio.
Msafara huo unatarajia kuondoka leo saa 10:00 jioni huku mkuu wa msafara akiwa ni Kaimu Rais wa Simba Dr. Salim Abdallah. Simba na Al Masry zilitoka sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
WAKATI HUO HUO.
AJIALI ya bodabda imemuondoa kikosini beki wa Simba, Salim Mbonde baada ya kuondolewa katika kikosi kinachosafiri nchini kesho kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry, Kombe la Shrikisho Afrika.
Simba itakuwa ugenini dhidi ya Al Masry katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Port Said mjini Port Said, Misri ikihitaji ushindi wowote kusonga mbele, baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Jumatano wiki iliyopita.
Beki huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji walikuwepo katika mipango ya Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre kumtumia katika mchezo huo kutokana na ajali hiyo iliyosababisha ashonwe nyuzi tatu juu kidogo ya jicho, amemuondoa katika mipango hiyo.
NAO,
Yanga watua salama mjini Gaborone, Botswana, jana mchana, wafikia hoteli yenye hadhi ya nyota mbili.
Kikosi hicho kitacheza dhidi ya Township Rollers FC, Jumamosi ya wiki hii, mchezo wa marudiano katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 Comments:
Chapisha Maoni