Mapadri wawili wa kanisa Katolika na waumini 16 wa kanisa hilo waliuawa katika shambulizi lililotokea katika kijiji cha Mbalom katika jimbo la Benue, nchini Nigeria.
Shambulizi hilo lililotokea katikati mwa nchi ambako kumeendelea kushuhudiwa mapigano ya kikabila limehusishwa wafugaji waliokua waibebelea silaha. Mashahidi wanasem ashambulizi hilo lilitokea mapena Jumanne asubuhi Aprili 24.
Washambuliaji hao waliingia katika kanisa wakati wa sherehe ya mazishi katika kijiji cha Mbalom, katika jimbo la Benue, nchini Nigeria. Mapadri wawili na waumini 16 wa kanisa Katoliki, wote waliuawa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na shirika la habari la AFP ambao pia wamesema watu wengi walijeruhiwa.
Washambuliaji pia walipora katika zaidi ya nyumba 60 na katika maduka ya chakula. Wakazi walikimbilia katika viijiji jirani kwa kuhofia usalama wao.
Dayosisi ya Makurdi, mji mkuu wa Jimbo la Benue, imelaani vurugu ambazo zilikumba mojawapo ya makanisa yake. Rais Muhammadu Buhari ameahadi kwamba wahalifu wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria kwa kutekeleza shambulizi lenye lengo la "kuchochea uhasama wa kidini".
Vijana wenye hasira walimiminika mitaani katika mji wa Makurdi kupinga hali hiyo kabla ya kutawanywa na polisi.
Washambuliaji wanadaiwa kuwa wafugaji, kwa mujibu wa mashahidi. Watu wamekua na wasiwasi ya kutokea mashambulizi ya ulipizaji kisasi katika jimbo hilo linalokumbwa na kwa miezi kadhaa na makabiliano mapya kati ya wakulima ambao ni kutoka kanisa Katolika na wafugaji ambao wengi wao ni kutoka jamii ya Peuls na Waislamu.
Jeshi ambalo lilitumwa mapem amwaka huu katika jimbo la Benue ambapo kunaripotiwa hali hiyo, halijafaulu kuzuia uhalifu.
0 Comments:
Chapisha Maoni