Halmashauli ya
mji wa kahama imewaagiza wafugaji wote
wanao jihusisha na ufugaji maeneo ya mjini kuondo mifugo yao mara moja na mifugo watakao onekana wakizulula ovyo
watakamatwa na kupigwa munada ndani ya siku saba.
Hayo ya
meelezwa na mkurugenzi mtendaji wa wahalmashauri ya mji wa kahama mjini Bwana Underson Msumba wakati ajibu maswali ya
madiwani juu ya mifugo inayo zulula ovyo maeneo ya mijini katika baraza la
majiwani lilofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa kahama mjini.
Aidha bwana Msumba ameeleza kuwa hairusiwi kwa
mfugaji yeyote kufuga mifugo maeneo ya mijini bila kibali na ufugaji unao
ruhusiwa ni ufugaji wa ndani ya zizi(0-grezing) na sio kuwatoa mifugo na
kuwapeleka malishoni maeneo ya mijini na kwamba mfugo wowote utakao kamatwa utatozwa
faini ya shilingi laki mbili.
Kwa upande
wake afisa mifugo wa halmashauri ya mji Bwana
Costantine Lugendo amesema kuwa kwa sasa wamekekwisha anza msako wa
kukamata mifugo wote katika kata zote kumi na moja na taayari zoezi hilo lipo
katika utekelezaji na kwa sasa zoezi lineendelea katika kata ya majengo na
nyahanga na linasimamiwa na watendaji wa kata na kwa kushirikiana na migambo.
Hata hivyo
baraza la madiwani la halmashauri ya mji
limeanza hii leo na na litamalizika april 24 mwaka huu na linajadili
utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopo katika halmashauri ya mji wa kahama.
0 Comments:
Chapisha Maoni