Familia mbili za watoto wanaosoma shule
ya sekondari Nyihogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga zimetakiwa kugharamia
uharibifu wa miundombinu ya madarasa ya shule ya msingi Nyihogo baada ya watoto
wao kuiharibu kwa kuandika matusi ya kuwatukana walimu wa shule hiyo ya msingi.
Akizungumzia hatua hiyo mwenyekiti wa
mtaa wa Bukondamoyo Frank Mabugi amesema baada ya uharibifu huo kufanywa
serikali ya mtaa imewataka wazazi wa watoto kugharamia sehemu iyoharibiwa kwa
kila familia kulipa kiasi cha shilingi 80,000 na ilipwe Februari 5, 2020.
Mabugi amesema sehemu iliyoharibiwa ni ukuta
wa vyumba viwili vya madarasa ambayo bado mapya toka yamekamilika kujengwa na
watoto waliofanya tukio hilo wanasadikika wamesoma katika shule hiyo ya msingi
Nyihogo ili kufidia uharibifu huo jumla ya fedha ni shilingi 160,000
inahitajika ambapo wazazi wa watoto hao watailipa.
Amesema wakati tukio hilo linafanywa na wanafunzi
kuandika matusi kuna baadhi ya watoto 23 ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi
Nyihogo waliwaona huku wakipewa vitisho ili wasitoe taarifa lakini licha ya
kupewa vitisho hivyo walisema na uongozi wa mtaa kuwabaini wazazi wao.
“Tumekutana na wazazi wa watoto hao
waliotuharibia miundombinu yetu na tumefikia muafaka kwanza tumeangalia
uharibifu wote na kuangalia gharama ya vifaa pamoja na malipo ya fundi na kiasi
cha shilingi laki moja na sitini elfu hivyo wameahidi kuilipa ili kufidia”.
Kwa upande wao wazazi wa watoto hao
wamesema kiukweli tabia hiyo sio nzuri na baada ya taarifa hizo ziliwashtushwa
hivyo kwa ujumla wanakiri kulipia gharama zote na watahakikisha tabia hiyo
haijirudii huku wakiwataka wazazi wenzao kuwa waangalifu kwa watoto.
0 Comments:
Chapisha Maoni