Serikali mkoani Shinyanga imevunja mkataba wa ujenzi wa barabara na mkandarasi wa Kampuni Ya THEMI INVESTMENT ya Dar es Salaam baada ya kushindwa kufanya kazi kulingana na mkataba.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi.Zainab Rajab Terack wakati akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa bodi ya barabara mkoa.
Amesema mkandarasi huyo amekuwa msumbufu wakati wa kutekeleza majukumu aliyopewa kwani alikuwa akisimamisha kazi bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika na kurundika vifusi kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa na usumbufu kwa wananchi.
Terack amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani Shinyanga kutowapatia tenda wakandarasi wasio kuwa na sifa kwani wanadumaza maendeleo ya mkoa na kuongeza kuwa miundombinu bora ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi.
0 Comments:
Chapisha Maoni