Jumla ya hisa milioni 16 zenye thamani sawa na dola ya kimarekani milioni 5.1 ziliuzwa katika soko la hisa la Nairobi (NSE) nchini Kenya siku ya jumanne.
Mauzo hayo yalikuwa pungufu ya malengo yaliyokadiriwa kutokana na wawekezaji wengi kuhamia masoko makubwa ya hisa na kutoa dhamana zao kwa mkopo, huku taifa hilo likielezwa kuchukua mkopo wa dola milioni 388 kwa ajili ya kusaidia bajeti.
Kampuni ya huduma za mawasiliano Safaricom, ndiyo ilikuwa rekodi ya mauzo ya siku hiyo, na kuuza jumla ya hisa zake milioni 6.9 zilizokuwa na thamani ya 0.29 kwa hisa moja, ikiwa ni ongezeko asilimia 0.8.
0 Comments:
Chapisha Maoni