Tume ya uchaguzi ya Russia imetoa taarifa kuwa, baada ya ukaguzi wa kikamilifu, tume hiyo imeamua kupitisha na kusajili wagombea wanane kwa ajili ya kumpata rais mpya wa Russia, akiwemo, rais wa sasa Vladimir Putin.
Habari zinasema, uchaguzi mkuu wa urais wa Russia utafanyika tarehe 18, mwezi ujao. Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwaka huu, warussia milioni 110 walikuwa tayari wamekwishapata haki ya kupiga kura.
Habari nyingine kutoka taasisi ya kukusanya maoni ya umma ya Russia imesema, hivi sasa, asilimia 69.9 ya watu, wanamuunga mkono Vladimir Putin kuendelea kuwa rais.
0 Comments:
Chapisha Maoni