Wakati shule hiyo ikifunguliwa Kamati maalum iliyoundwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai na kubaini chanzo cha matukio ya mara kwa mara na utovu wa nidhani katika shule hiyo imewasilisha ripoti yake na hatua za kuchukua.
Wanafunzi 890 walilazimika kuja na wazazi wao katika ofisi ya Mkuu wa shule huku wakiwa na barua katika maeneo wanayotoka.
Uongozi wa shule hiyo umechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwafukuza wanafunzi 7 wa kidato cha Tano lakini pia kuwasimamisha kwa muda wanafunzi wa kidato cha sita ambao watalazimika kufika shuleni siku ya mitihani ya Kitaifa ya kitado cha sita.
Jengo ambalo liliharibiwa liliharibiwa vibaya na wanafunzi hao limeanza kufanyiwa matengenezo huku likidaiwa kugharimu karibu Milioni 6 ambazo zinatokana na michango mbalimbali ambayo imechangwa na wanafunzi kwaajili ya mahafali.
0 Comments:
Chapisha Maoni