Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchini FAT ambacho kwa sasa ni shirikisho Ismail Aden Rage ameutaka uongozi wa shirikisho hilo kubadili mfumo wa kuitengeneza timu ya taifa (Taifa Stars) kwa lengo la kuondoka hapa tulipo na kufika yalipo mataifa mengine duniani yenye mafanikio.
Rage ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba amesema kwa miaka mingi Tanzania imekua ikitumia mfumo wa kukurupuka na kushindwa kuwa na kikosi imara cha Taifda Stars, hivyo anaaona muda wa kubadilika umefika kwa kuwahimiza viongozi wa TFF kubadili mfumo.
Amesema tunapaswa kuiga mfumo wa taifa kubwa katika soka Ujerumani ambalo ndio bingwa wa dunia kwa sasa, kwa kuangalia namna walivyokijenga kikosi chao ambacho mwaka 2014 kiliushangaza ulimwengu kwa kuichapa Brazil mabao saba na badae kutwaa ubingwa.
Hata hivyo Rage amewataka wachezaji wa soka wa wakati huu kutambua tahamani wa mchezo wa soka ili kuvipa heshima vilabu vyao pindi wanapoitwa katika timu ya taifa, kama ilivyokua miaka ya 1970 wakati akilisakata kabumbu akiwa na klabu ya Simba.
Rage amesema wachezaji wengi wanaozitumikia klabu za Simba na Young Africans wamekua akiamini kuwa ndani ya klabu hizo ni njia sahihi ya kuitwa katika timu ya taifa, lakini wanashindwa kujua thamani waliyonayo na sehemu waliopo.
Katika hatua nyingine Rage amewataka wadau wa soka kuacha kuinyooshea kidole Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kisingizio inashindwa kuingia moja kwa moja katika michezo, na badala yake wameshauri sheria ya kuchangia katika michezo irudishwe ili kuiwezesha Taifa Stars na timu nyingine za taifa kufanya vyema.
0 Comments:
Chapisha Maoni