Rais Raul Castro wa Cuba jana alikutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye yuko ziarani nchini humo, na viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya nchi hizo.
Rais Castro ameishukuru serikali ya Kenya kwa kuiunga mkono na msaada wake iliotoa wakati wa maafa ya Kimbunga Irma kilichokumba pwani ya kaskazini ya Cuba mwaka jana, ambacho kilisababisha hasara ya zaidi ya dola bilioni 13 za kimarekani.
Mapema siku hiyo, rais Kenyatta alizindua sanamu ya hayati baba yake ambaye pia ni rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta katika bustani moja mjini Havana.
Rais Uhuru ameishukuru Cuba kwa mshikamano wake na nchi za Afrika, na kusema daima Afrika itadumisha uhusiano wake na Cuba.
Marais hao pia wameeleza kuridhishwa na ufunguzi rasmi wa ubalozi wa Kenya mjini Havana, ambao unatarajiwa kufanyika hii leo.
0 Comments:
Chapisha Maoni