MBAO WAWASILI SALAMA MWANZA, RATIBA YA MAZOEZI HII HAPA.

Image result for mbao fc

Timu ya Mbao Fc iliwasili juzi salama ikitokea Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Azam Fc. Kwa sasa timu inaendelea na kambi ya mazoezi iliyopo katika chuo cha ualimu butimba.


MAJERUHI.
Wachezaji wote wapo katika hali nzuri kiafya isipokuwa kiungo Husein Kassanga Chuse ambaye anauguza majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyopata kwenye mechi dhidi ya singida United. 


Mchezaji Yusuph Mgeta aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti afya yake imeimarika na anaendelea na mazoezi.

MAZOEZI.
Kwa mujibu wa programu ya mwalimu timu itakuwa ikifanya mazoezi kuanzia saa kumi jioni. 


Na wakati mwingine itafanya mazoezi asubui na jioni, hii itategemea mahitaji ya mwalimu. Uwanja wa mazoezi ni butimba na CCM kirumba (kwa wakati fulani).

MWISHO.
Bodi pamoja na uongozi wa Mbao Fc unatoa shukrani kwa wanamwanza hususani waandishi wa habari kwa ushirikiano mnaotupatia. 


Kwetu sisi kukosolewa ni silaha muhimu katika kujiimarisha. 

Imetolewa na:
Daniel Naila
Katibu Mbao Fc
0745531590
0626014026
Email: danielnaila@saut.ac.tz
              mrawadaniel@yahoo.com
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni