Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga inakabiliwa na upungufu wa madawati 1720 kwa shule za sekondari.
Hayo yamebainishwa na afisa elimu vifaa na kazi wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Bw. Seleka Ntobi wakati wa makabidhiano ya madawati kutoka mfuko wa mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige.
Ntobi amesema kuwa mahitaji ya madawati kwa halmashauri ya Msalala ni 9187,yaliyopo ni 7467 hivyo kuwa na upungufu wa madawati 1720 kwa
shule za sekondari na shule za msingi zikiwa na upungufu wa madawati 734.
Ili kupunguza changamoto ya madawati katika halmashauri ya Msalala ofisi ya mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige kupitia mfuko wa jimbo umetoa jumla ya madawati 180 .
Katibu wa mbunge wa Msalala Jackson Lutego amesema kuwa madawati hayo ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi ambapo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 12.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Leonard Mabula ameipongeza ofisi ya mbunge kwa kutoa msaada wa madawati hayo
huku akitoa wito kwa wadau wengine wa elimu ikiwa ni pamoja na taasisi binafsi kuendelea kuchangia katika sekta ya elimu ili kumaliza hangamoto shuleni.
Na. Faustine Gimu Galafoni,Kahama.
0 Comments:
Chapisha Maoni