Sekretariati ya Shirikisho la soka Tanzania TFF ilimfikisha Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kwenye kamati ya maadili akikabiliwa na tuhuma tatu ikiwemo kupokea fedha za malipo TFF za malipo ambayo hayakuwa halali.
Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TFF, baada ya kamati ya maadili kupokea malalamiko yanayomhusu Wambura na kukutana jana (Machi 14, 0218) kwa ajili ya kujadili, imemfungia maisha Wambura kujihusisha na masuala ya soka.
Kwa mujibu wa afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo, Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo, kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi. Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea.
Emanuel Muga amesema hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14, 2018).
“Ni kweli sikupewa nafasi ya kumtetea kwa sababu kamati ilikuja ikiwa na dhamira yake kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo. Kwa hiyo nilivyowasilisha masuala ya kisheria ambayo ni ya kikanuni, kamati ilikataa ikasema sisi tunaamua tunavyoona”-Emanuel Muga, Wakili wa Wambura.
“Kwa hiyo wakalifunga suala kwamba yanaenda kufanywa maamuzi, lakini hayo maamuzi yatafanyika wakati Wambura hajasikilizwa na Wakili wake hajasikilizwa.”
0 Comments:
Chapisha Maoni