AU NA EU ZAUNGANISHA NGUVU KUISAIDIA AFRIKA YA KATI.



Umoja wa nchi za Afrika (AU), pamoja na Umoja wa Mataifa wameanzisha tena ushirikiano madhubuti ili kurejesha amani na utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), wakati huo huo wakiendelea kuwalinda raia wa nchi hiyo dhidi ya mitandao ya kihalifu.

Taasisi hizo mbili zimehimiza uhitaji wa kuendelea kuvisaidia vikundi vya kijamii, vikundi vya wanawake, viongozi wa kidini na makundi mengine ndani ya ambao wanatetea amani katika nchi hiyo.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika jana ijumaa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika, Kamishna wa AU anayeshughulikia masuala ya amani na usalama, Ismail Chergui, na msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, anayeshughulikia michakato wa kulinda amani, Jean Pierre Lacroix, wameeleza masikitiko yao juu ya kuendelea kwa migogoro katika maeneo ya jirani na mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Wawili hao walifanya ziara ya pamoja ya siku tatu kuanzia April 10 hadi 12 huko Bangui ambako walikutana na kufanya majadiliano na maafisa wa serikali, wawakilishi wa vikundi vya kijamii, vikundi vya wanawake pamoja na viongozi wa kidini.

Kutokana na mikutano waliyofanya kwenye ziara hiyo, wawili waliwaambia waandishi wa habari kuwa, wanavikundi hao wanahitaji msaada wa kufikia malnego yao ya kudumisha amani kwa kuwa tayari wanao ujumbe na wako tayari kwa maridhiano na amani na majadiliano.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni