TIC YAKARIBISHA WAWEKEZAJI NCHINI TANZANIA.

Serikali ya Tanzania kupitia kituo chake cha kuendeleza uwekezaji 'TIC' imewakaribisha wawekezaji zaidi kutoka nchini China kwenda kuwekeza Tanzania, na kwamba kituo hicho kitawasidia kufanikisha na kurahisisha shughuli zao.

TIC ndio wakala mkuu wa serikali ya Tanzania inayoshughulikia masuala ya kuratibu, kuwezesha, kendeleza na kusimamia uwekezaji nchini Tanzania, na ndio chombo chenye mamlaka ya kuishauri serikali kuhusu masuala yoyote yanayohusiana na uwekezaji.

Akizungumza katika mahojiano maalum na shirika la habari la Xinhua mkurugenzi mkuu wa TIC, Geoffrey Mwambe, amesema kwa kuwa serikali ya Tanzania kwa sasa inaangazia zaidi uwekezaji kwenye viwanda, hivyo amewashauri makampuni mengi ya China kwenda kuwekeza akitolea mfano baadhi ya makampuni ya China ambayo tayari yameanza kufanya hivyo.

Kitakwimu za uwekezaji, Bw. Mwambe amesema biashara kati ya Tanzania na China imeendelea kukua vizuri, akisema China itabaki kuwa mshirika mkubwa zaidi wa Tanzania katika biashara ambapo pato la biashara hiyo ikikadiriwa kufikia dola za kimarekani bilioni 3.88 kwa mwaka 2016.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo ameishukuru China kwa kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kipaumbele katika ushirikiano wa China na Afrika.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni