KIM NA MOON WANAKUTANA LEO, YATAZAMIWA KUWA MAZUNGUMZO YA KIHISTORIA.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na mwenzake wa Korea Kusini, Moon Jae-in wamekutana na kufanya mazungumzo mapema leo Ijumaa katika kijiji cha Panmunjom kwenye eneo la mpaka wa nchi hizo mbili la Demilitarized. Mazungumzo haya yanatajwa kuwa ya kihistoria.
Mazungumzo hayo ni ya kwanza baina ya viongozi wa Korea mbili katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita. Kwenye mazungumzo hayo Rais wa Korea Kusini ametoa wito wa kufikiwa "makubaliano ya kijasiri" baina ya pande hizo mbili.
Moon Jae-in amesema anatarajia kwamba pande mbili zitafikia makubaliano ya kijasiri na kuwapa zawadi watu wote wa Korea na wale wanaopenda amani.  
Baada tu ya viongozi hao kuamkuana, Kiongozi wa Korea Kaskazini alimuomba mwenzake wa Korea Kusini avuke mpaka na kuingia upande wa Korea Kaskazini na kisha wote wawili walivuka tena mpaka na kuingia Korea Kusini. 
Viongozi hao wa Korea mbili wanajadili na kubadilishana mawazo kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Peninsula ya Korea na jinsi ya kudhamini amani ya kudumu na hali bora kwa watu wa nchi hizo mbili jirani na mahasimu wa miaka mingi.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni