SHAHID KHAN: BILIONEA ANAYETAKA KUUNUNUA UWANJA WA WEMBLEY.


Shahid Khan ndio jina ambalo siku ya leo limetawala vyombo vingi vya habari nchini Uingereza, jina la Shahid linaongelewa sana baada ya kutoa ofa kwa chama cha soka Uingereza ya kutaka kuununua uwanja wa Wembley.

Khan ni mzaliwa wa familia ya kisomi nchini Pakistan katika mji wa Lahore ambapo mama yake alikuwa ni profesa wa somo la Hisabati nchini mwao na baba yake akiwa mfanyabiashara nchini mwao.

Sasa Shahid ambaye ni mmiliki wa klabu ya Fulham pamoja na timu inayoshiriki NFL ya Jacksonville Jaguars ameweka mezani kiasi cha £800m kwa ajili ya kuununua uwanja wa taifa wa Uingereza Wembley.
FA wameipokea ofa hiyo na wameanza kuijadili na kupitia kwa msemaji wa chama cha soka Uingereza wamethibitisha kwamba wamepokea ofa hiyo ya uwanja huo ambao mwanzo ulitajwa kuwa na thamani ya £757m.



Hapo mwanzo Khan aliomba kuwa awe anaileta timu yake inayocheza “American Football” katika uwanja wa Wembley walau mara moja kila mwezi, lakini sasa inaonekana anataka kuihanisha kabisa NFL ije Wembley.

Nini hatma ya timu ya taifa ya Uingereza? Inafahamika kwamba uwanja wa Wembley ndio uwanja wa timu ya taifa ya nchini Uingereza, na swali hili limekuwa likulizwa sana mitandaoni kwamba nini kitatokea kama Wembley ikinunuliwa.

Japokuwa vipengele vya mkataba wa uuzwaji wa Wembley kati ya FA na Khan haujawekwa wazi, lakini inaonekana kwamba kati ya jambo ambalo halitabadilika ni timu ya taifa ya Uingereza kuutumia Wembley, na Khan akiununua bado Uingereza watabaki Wembley.
Chelsea nao watahamia vipi Wembley? Chelsea nao wanataka kuhamia Wembley wakati Stamford Bridge ikiwa katika matengenezo, na suala la Chelsea bado hadi sasa hakuna habari ya uhakika kwamba nini kitatokea kwao kama Wembley itanunuliwa.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni