Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajia kuzuru Marekani Jumatatu hii. Hii ni ziara rasmi ya kwanza kwa rais wa nchi ya Afrika tangu Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua madaraka nchini Marekani.
Ziara hii ya Buhari inakuja miezi kadhaa baada ya Rais Donald Trump kukashifu mataifa ya Afrika.
Kwa kawaida, ofisi ya rais nchini Nigeria haikuweza kutoa taarifa hii, kwani ilikua ilisalia kama siri kubwa kwa taifa hilo. Kwa mujibu wa ikulu ya White House, mazungumzo kati ya wawili hao yatajikita kuhusu vita dhidi ya ugaidi, usalama na uchumi.
Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kutoka bara la Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House atakapokutana na kiongozi huyo kwa mashauriano rasmi mjini Washington.
Marais wengine wa Afrika waliwahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, ni Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, lakini nje ya Marekani.
Ziara ya Rais Muhammadu Buhari inakuja ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Nigeria.
0 Comments:
Chapisha Maoni