WAZEE WA KIMILA TANZANIA NA KENYA KUKUTANA TARIME, NI KUHUSU UKEKETAJI.




Baada ya kuungana ili kutoa elimu na kupinga vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike,Wazee wa koo12 Wilayani Tarime Mkoani Mara wamesema  kuna haja ya kukutana na kufanya kikao na wazee wa mila kutoa nchi jirani ya Kenya ili nao kupata elimu hiyo.

Wangubo Mtongori ni mzee wa Mila kutoka koo ya Bukira na Mjumbe wa Muungano huo wa wazee wa Mila Wilaya ya Tarime amesema kuwa kama wao upande wa Tarime wameamua kuungana na kukemea Ukeketaji lakini kuna baadhi ya koo zao zinaenda mpaka nchi jirani ya Kenya kuna haja sasa ya kukutana nao ili nao wapewe Elimu Mtoto asije toka Tanzania kwenda Kenya kukeketwa.

“Mimi ni Kiongozi kwa upande wa Kenya kwa sababu koo ya Bwirege Nyabasi na Wakira ni baadhi ya koo ambazo zinaungana Kenya sasa hawa wenezetu wa Kenya hawajapata hii elimu wanaweza kushuiriki kukeketa watoto wetu na likaleta doa tena ni bora serikali isaidi kutukutanisha pia na wenzetu ili nao wapewe elimu na sisi tuwambie kuwa tumeacha kukeketa mtoto wa kike” alisema Wangubo.

Afisa Ustawi wa Jamii Afya Tarime, Abel Gechaine  amesema  nia ya serikali siyo kuondoa mila zote bali wanaangalia Mila zenye dosari huku akiwaomba wazee wa Mila hao kuruhusu kuleta wataalamu kipindi cha Tohara ili kuhakikisha kuwa Msichana hajakeketwa bali amepakwa unga usoni kwa lengo la kutimiza mila na kuendelea na sherehe zao na kula chakula na kunywa togwa.

“Sisi Serikali tunachopinga ni kile kitendo cha kukeketa binti lakini kama ni masuala ya kutimiza mila sisi hatuna shida ila sasa wazee wangu niwaombee siku hiyo mkaruhusu tulete wataalamu yaani Manesi ili kitendo hicho kinafanyika wanashudia” alisema Gechaine.

Mkurugenzi Mtendaji shirika la ATFGM Masanga ambao wanapiga Vita ukatili wa kijinsia Ukiwemo Ukeketaji,Sister Stella Mgaya alisisitiza suala la kupeleka watoto wa kike shule badala ya kuwaozesha huku Afisa Mtendaji wa kijiji cha Itiryo Veronica Elias akipongeza wazee haoa kwa kufikia hatua ya kutoa tamko juu ya suala la kuacha ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

Kwa sasa wazee wa Mila koo12 Tarime wameungana pamoja kwa lengo la kupiga vita suala la ukeketaji na kuondoa mila potofu zilizokutwa na wakati.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni