Kocha wa timu ya Ujerumani
Joachim Loew amekitangaza kikosi cha awali cha Kombe la Dunia, ambalo litang'oa
nanga Urusi mwezi Ujao huku DFB pia imerefusha mkataba wa kocha huyo hadi 2022.
Hatua ya kuurefusha mkataba
wa Löw sio ya kushangaza kwa sababu Rais wa Shirikisho la Kandanda Ujerumani –
DFB Reinhard Grindel alikuwa amesema awali kuwa kocha huyo ataendelea kuiongoza
timu ya taifa, hata kama Ujerumani itaondolewa katika robo fainali ya Kombe la
Dunia la Urusi. Mikataba ya kocha msaidizi Thomas Schneider na mwalimu wa
makipa Andreas Köpke pia imerefushwa hadi 2022.
Mkataba wa mkurugenzi wa
DFB na meneja mkuu wa timu ya taufa Oliver Bierhoff imerefushwa hadi 2024.
Kocha wa timu ya Ujerumani
Joachim Loew amekitangaza kikosi cha awali cha Kombe la Dunia, ambalo litang'oa
nanga Urusi mwezi Ujao. DFB pia imerefusha mkataba wa kocha huyo hadi 2022.
Kocha wa timu ya taifa ya
kandanda ya Ujerumani Joachim Löw amekitangaza kikosi cha wachezaji 27, ambao
wataandamana naye kwa ajili ya kambi ya mazoezi nchini Austria wiki ijayo. Hii
ina maana kuwa atahitajika kuwapunguza wachezaji wanne kutoka kwa orodha hiyo
kabla ya kuelekea Urusi kwa dimba la Kombe la Dunia.
Kando na kuachwa nje kwa
kiungo wa Borussia Dortmund Mario Götze, aliyefunga bao la ushindi la Ujerumani
katika kombe la dunia nchini Brazil, hakukuwa na majina mengine ya kushangaza
kikosini, ambacho kilitangazwa Alhamisi katika jumba la makumbusho ya kandanda
la Ujerumani mjini Dortmund.
Kuna waliokuwa na maswali
ya kama kipa nambari moja Manuel Neuer atachaguliwa, ikizintaiwa kuwa hajacheza
mechi yoyote ya ushindani tangu Septemba kutokana na maumivu ya mguu.
Hata hivyo, jina la Neuer
lipo kwenye orodha hiyo, mmoja wa makipa wanne watakaosafiri kwenda Austria. Nils
Petersen amechaguliwa badala ya Sandro Wagner.
Kikosi cha awali cha Ujerumani:
· Goalkeepers.
Bernd
Leno
(Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter
Stegen
(Barcelona), Kevin Trapp (Paris Saint-Germain), Manuel Neuer (Bayern Munich)
· Backs.
Jerome
Boateng (Bayern Munich), Matthias
Ginter (Borussia
Moenchengladbach), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Marvin Plattenhardt (HerthaBerlin), Antonio Ruediger (Chelsea), Niklas Suele (Bayern Munich), Jonathan Tah (Bayer Leverkusen)
·
Midfilders.
Julian
Brandt (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Paris
Saint-Germain), Leon Goretzka (Schalke), Ilkay Guendogan (Manchester City), Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Thomas Mueller (Bayern Munich), Mesut Oezil (Arsenal), Sebastian Rudy (Bayern Munich), Leroy Sane (Manchester City), Marco Reus (Borussia Dortmund)
·
Attackers.
Timo
Werner (Leipzig), Mario
Gomez (Stuttgart), Nils Petersen
(Freiburg.)
0 Comments:
Chapisha Maoni