Kampuni ya Great Lakes Africa Energy (GLAE) imeingia mkataba na serikali ya Msumbiji wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani wa gharama ya Sh40 bilioni ($400 million).
Kampuni hiyo ya Uingereza inajenga na kuendesha miradi ya umeme katika eneo la jangwa la Sahara.
Makubaliano hayo ya ujenzi wa kiwanda cha umeme wa gesi cha megawati 250 yalitiwa saini ijumaa iliyopita mjini Maputo.
Msumbiji ambayo ina gesi asilia kwa viwango vikubwa imeamua kutumia gesi hiyo kwa ajili ya miradi ya umeme ili kupata ukuaji endelevu wa uchumi.
0 Comments:
Chapisha Maoni