KAMPUNI ZA SIMU ZATAKIWA KUHAKIKI WATUMIAJI.

Baraza la ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC),limezitaka kampuni za simu kutimiza wajibu wao wa kisheria kwa kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mitandao hiyo dhidi ya wahalifu.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wahalifu wa mitandao ambao wanatumia simu za mikonono kutuma jumbe mbalimbali za kuomba fedha na utapeli jambo linalosababisha usumbufu kwa watumiaji wa huduma hizo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa TCRA-CCC,Mary Msuya,amesema kumekuwa na malalamiko yanayotolewa na watumiaji wa mitandao wanaopokea kupitia simu za mikononi na kwenye mikutano.

Amesema matukio hayo yamekuwa na wahalifu wanaomiliki namba za simu zilizosajiliwa na kampuni za mitandao mbalimbali.

Amesema katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Januari mwaka huu,wamepokea simu za watumiaji wa mitandao 103 wakilalamikia kupokea ujumbe wa kitapeli.

Pia amesema matukio hayo yameshamiri katika kipindi cha kuanzia mwaka huu na kwamba mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom namba zake huwa zinatumiwa zaidi ya mitandao mingine.

Aidha amesema wanachofanya kama TCRA-CCC,ni kutoa elimu na ushauri kwa watumiaji wa mitandao kabla ya kukumbwa na uhalifu huo na ikitokea mtumiaji ametapeliwa suala hilo wanaliachia jeshi la polisi.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni