Rais wa Ghana Akufo Addoa metoa amri
ya kukamatwa kwa Rais wa Ghana Football Association (GFA), Kwesi Nyantakyi
ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa shirikisho la soka Afrika Caf.
Nyantakyi anatuhumiwa kufanya
udanganyifu na ufisadi kwa kutumia jina la Rais la Rai wa Ghana Akufo Addoa.
Amri ya Rais Addo imekuja baada ya
mwandishi wa habari Anas Aremeyaw kuibua udanganyifu na ufisadi wa Nyantekyi
kupitia makala yake ya uchunguzi.
Uchunguzi huo pia unadaiwa kufichua
vitendo vya ufisadi miongoni mwa maafisa wengine wa shirikisho la soka nchini
Ghana.
Video hiyo inapangiwa kuoneshwa kwa
wananchi Juni 6, 2018 lakini inadhaniwa Rais wa Ghana ameiona kabla ya kutoa
amri ya kukamatwa kwa Nyantenkyi.
Kwesi Nyantenkyi amekuwa rais wa
shirikisho la kandanda nchini Ghana tangu mwaka 2005 na hajatamka lolote.
0 Comments:
Chapisha Maoni