Ikiwa leo ni kilele
cha maadhimiso ya siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia shirika lisilo la kiserikali lililopo mkoani
shinyanga the voice of magenalized
community [TVMC] LImefanya Tamasha
katika uwanja wa SHY COM mkoani hapo.
Katika maadhimisho
haya mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala
msaidizi mkoa wa shinyanga JOAKIM OTARU katika hotuba yake
ameeleza dhumuni la kuadhimisha maadhimisho haya yamekuwa kichocheo cha
mabadiliko ya maboresho ya sera na mikakati mbalimbali ya kumuinua na kumkomboa mwanamke katika Nyanja mbalimbali ambapo amesema kumekuwepo na sera ya
maendeleo ya wanawake na jinsia ya
kuwainuwa wanawake kiuongozi, kiuchumi
ukiwemo mpango kazi wa taifa katika
kudhibiti ukatili wa kijinsia dhidi
ya wanawake na watoto yaaini MTAKUWA.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga
Bwana MFINANGA JOHN ameeleza takwimu za kesi za unyanyasaji wa kijinsia ambapo wilaya ya kahama
inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia huku akitaja
jumla ya kesi 314 zipo katika upelelezi kati ya kesi 470 zilizolipotiwa.
Katika maadhimisho hayo
wageni mbalimbali pamoja na taasisi
zisizo za kiserikali, ikiwemo HUHESO FOUNDATION, AGAPE, WFT, Viongozi wa dini, watendaji ofisi ya mkoa, dawati la jinsia mkoa wa shinyanga na wanafunzi
kutoka shule mbalimbali wameshiriki
ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kizazi chenye usawa simamia dhidi ya ubakaji.
Na Halima Hassan
0 Comments:
Chapisha Maoni