Jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia katika halmashauri ya
mji wa Kahama mkoani Shinyanga limesema katika kushughulikia matukio ya
kikatili limekuwa likikabiliwa na changamoto ya mashahidi kutokufika mahakamani
pamoja na wahanga wa matukio hayo kutoroshwa.
Akisoma risala
kwa mgeni rasmi mkaguzi msaidizi wa polisi dawati la jinsia Zainabu Mangala
amesema kumekuwa na changamoto kadhaa ndani ya jeshi katika kutekeleza majukumu
yake miongoni ni kukosa gari la kusaidia kufika katika matukio kwa wakati.
Kwa upande wake
afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji wa Kahama Robert Kwela amesema
katika kipindi cha nusu mwaka 2019 kuanzia mwezi Julai hadi Disemba ofisi yake
imepokea mashauri ya ukatili 651 na kwa kushirikiana na jeshi la polisi
yamefanyiwa kazi.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha
amesema licha ya changamoto hizo kulikabili jeshi la polisi analiomba lisikate
tamaa kushughulikia matukio ya ukatili kwani yanapaswa kukomeshwa katika jamii.
Na Paschal Malulu
0 Comments:
Chapisha Maoni