Deni la nje la Kenya limeongezeka katika miezi iliyopita na kuzidi dola bilioni 45 za kimarekani wakati serikali ya nchi hiyo inayokabiliwa na uhaba wa fedha ikiongeza kasi ya kukopa.
Ripoti ya robo mwaka ya tathmini ya uchumi na bajeti iliyotolewa na hazina ya nchi hiyo imesema, mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana, deni hilo lilifikia dola za kimarekani bilioni 45.1.
Mwishoni mwa mwaka 2016, deni la nchi hiyo lilikuwa ni dola za kimarekani bilioni 38, na mwaka jana, serikali iliongeza kasi ya kukopa kutoka vyanzo vya ndani na nje ya nchi hiyo.
0 Comments:
Chapisha Maoni