POLISI UGANDA YAANZA KUCHUNGUZA MAUAJI YA RAIA WA KIGENI.

Polisi nchini Uganda wameanza uchunguzi wa vifo vya raia wawili wa Ulaya vilivyotokea mjini Kampala wiki iliyopita.

Msemaji wa jeshi la polisi la nchi hiyo Emillian Kayima amesema, raia mmoja wa Uingereza anashukiwa kujiua katika nyumba aliyopanga kwenye eneo la watu matajiri jumatatu wiki iliyopita, na mwanaume mwingine raia wa Ujerumani amefariki akiwa hospitali ijumaa iliyopita, siku mbili baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana.

Marehemu hao walikuwa kati ya raia 6 wa nchi za magharibi waliokutwa wamekufa nchini Uganda katika siku 20 zilizopita. 

Wachunguzi nchini humo wamesema vifo hivyo huenda vimetokana na dawa za kulevya au mshtuko wa moyo.
Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni