LUKUVI: MARUFUKU KUMILIKI ARDHI ZAIDI YA EKARI 50.


Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amepiga marufuku kwa kijiji chochote hapa nchini kumilikisha ardhi kwa mtu binafsi zaidi ya ekari 50 bila idhini ya Rais.

Akizungumza na wananchi wa Kahama katika kampeni maalum aliyoianzisha ya Funguka kwa waziri yenye lengo la kupunguza na kumaliza migogoro ya ardhi hapa nchini ,Waziri Lukuvi amesema kuwa mara nyingi viongozi wamekuwa chanzo cha migogoro kwa kuwapa watu maarufu ardhi.

Waziri Lukuvi amepata fursa ya kusikiliza jumla ya kero 700 za migogoro ya ardhi wilayani Kahama kwa muda wa masaa  12 mfululizo kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa tatu usiku ambapo kila mwananchi
ametoa kero yake juu ya migogoro hiyo.

Lukuvi amesema ili kupunguza migogoro ya ardhi wizara yake inafanya marekebisho mfumo kwa mabaraza ya ardhi kote nchini ili kuwaondolea
maumivu wananchi .

Waziri Lukuvi ameendelea na ziara yake wilayani Kahama hususan kutembelea kwenye maeneo husika yenye migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na chuo cha Maendeleo ya Jamii Mwamva  na kuweza kuyatatulia
ufumbuzi .

Share on Google Plus

About huhesofm blog

0 Comments:

Chapisha Maoni