Rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kumpendekeza bungeni hii leo, mwenyekiti wa chama cha Christian Demoratic Union-CDU, Angela Merkel achaguliwe tena kuwa kansela. Zoezo kamili la kuchaguliwa Merkel na kuapishwa baraza jipya la mawaziri linapangwa kuzekelezwa Marchi 14 inayokuja.
Kura ya ndio ya SPD imewashusha pumzi sio tu wana SPD na wahafidhina wa CDU/CSU, bali pia rais wa shirikisho Steinmeier."Ni jambo la maana kwa nchi yetu, kwamba hali hii ya kutokuwa na uhakika wala yakini sasa imetoweka."Amesema rais wa shirikisho.
Katibu mkuu wa chama cha kansela Merkel, CDUAnnegret Kramp-Karrenbauer ana matumaini mema anasema:"Tutashirikiana vizuri bila ya shaka na SPD. Wamehapata uungaji mkono mpana wa mashinani. Tuna mkataba wa serikali ya muungano uliofafanuliwa vyema. Huo ndio msingi wa majukumu yetu, na unabidi ufuatwe. Zaidi ya hayo kuna uwanja mpana uliosalia na ambao kila chama kinaweza kuutumia kuendeleza mipango yake wenyewe."Ujerumani yashusha pumzi baada ya SPD kusema ndio
Wakati huo huo viongozi wa vyama hivyo vitatu, CDU/CSU na SPD, wanakutana, kila mmoja upande wake kujadiliana kuhusu hatua za mwisho mwisho za kuunda serikali. Viongozi wa CDU wanakutana mchana huu mjini Berlin.
Sambamba na hayo viongozi wa CSU wanakutana nao mjini Munich kuzungumzia nani wakabidhiwe wadhifa gani katika serikali mpya ya muungano.
Duru za karibu na mkutano huo zinasema Horst Seehofer atajiuzulu Marchi 13 kama waziri mkuu wa jimbo la kusini la Bavaria .
Seehofer anatarajiwa kukabidhiwa wizara ya mambo ya ndani katika serikali mpya.
SPD wanapanga kutangaza majina ya watakaokabidhiwa nyadhifa za mawaziri siku zinazokuja.
Jumla ya wizara sita zitaongozwa na SPD miongoni mwao ni wizara ya mambo ya nchi za nje, fedha na ajira.
Kinachojulikana kwa uhakika ni kwamba mwenyekiti mteule wa SPD, Olaf Scholz ndie atakaekuwa naibu kansela na kukabidhiwa wizara ya fedha.
Kama Sigmar Gabriel ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje bado haijulikani."Serikali mpya ya muungano wa vyama vikuu-GroKo inabidi iwajibike zaidi" amesema Jens Spahn wa chama cha CDU.
Vyama vya CDU/CSU na SPD vimepoteza idadi kubwa ya wapiga kura, la muhimu kwa sasa ni kurejesha imani ya wapiga kura amesisitiza.
Hatima ya Sigmar Gabriel kama waziri wa mambo ya nchi za nje haijulikani.
0 Comments:
Chapisha Maoni