Mshambuliaji Meddie Kagere amesema yuko na anatarajia
kucheza timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi
kwa mara nyingine tena.
Kagere, mwenye umri wa
miaka 32, ambaye sasa anacheza soka la kulipwa nchini Kenya Gor Mahia,
ameyasema hayo jana baada ya kukamilisha mchakato wake wa kuchukua uraia wa
kisoka nchini humo rasmi.
Kagere, alizaliwa Uganda, wazazi
wake ni wanyarwanda wanaoishi Uganga, na jana rasmi amerejea nyumbani kuongeza
nguvu Amavubi.
Kagere, ambaye alicheza kwa
mara ya kwanza Amavubi mwaka 2011 na alifunga mabao kumi katika michezo kumi ya
timu ya taifa, alikuwa mmoja wa wachezaji waliopoteza uraia miaka michache
iliyopita baada ya kuwa wachezaji wengi wa kigeni na sasa amepata kibali rasmi
cha kuichezea Rwanda.
Uamuzi wa kujiondoa uraia nchini
humo kulitokana na washambuliaji zaidi ya 60 kujiondoa baada ya Rwanda kufutwa
katika mechi za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 kwa kumtumia mchezaji mwenye uraia
wan chi mbili wa Congo, Dady Birori,
ambaye pia ana pasipoti ya Kongo chini ya jina la Agiti Tady Etakiama.
Kagere hapo awali alicheza
vilabu kadhaa vya Rwanda, ikiwa ni pamoja na Rayon Sports, SC Kiyovu Police FC
na Atraco FC sasa. Pia alicheza Mbale ya Uganda na Masaka LC, pamoja na Tunisia
wa Esperance Sportive de Zarzis.
Wengine waliomaliza
mchakato wao wa uhamiaji wiki hii ni pamoja na Hussein Cyiza (Mukura), Jimmy
Mashingirwa 'Mbaraga' Kibengo (AS Kigali), Andre Fils Lomami (Kiyovu) na Peter
Kagabo 'Otema (Musanze).
Ligi ya Rwanda inaendelea
na sasa ina michezo 17 na APR ndiye anayeongoza akiwa na point 34.
WAFUNGAJI.ational Football league top Scorers
- Ndarusanze
J. Claude (AS Kigali) 9
- Mutebi
Rashid (Mukura VS) 7
- Songa
Isaie (Police Fc) 6
- Uwimbabazi
Jean Paul (Kirehe) 6
- Kakule M.
Fabrice (SC Kiyovu) 6
- Bahame
Arafat (Marines Fc) 5
- Hakizimana
Muhadjiri (APR Fc) 5
- Bokota
Labama (Musanze Fc) 5
- Wayi Yeka
(Musanze Fc) 5
- Ruhinda
Farouk (Bugesera Fc) 5
- Mumbere
Claude (Etincelles Fc) 5
- Orotomal
Alex (Sunrise Fc) 5
0 Comments:
Chapisha Maoni