Paul "Latest"
Nkata amejiuzuru kuwa kocha mkuu wa watoza ushuru wa Uganda URA FC Jumanne
jioni.
Hii ilitokea baada ya URA
kupewa kichapo kama mwizi aliyeiba stendi 7-2 na mabingwa watetezi, Kampala
Capital City Authority (KCCA).
Mkurugenzi Mtendaji (CEO), wa
URA Edward Kulubya alithibitisha katika kwa vyombo vya habari;
Nkata alijiunga na URA
kuelekea mwishoni mwa mzunguko wa kwanza mnamo Desemba 2017, akichukua nafasi
ya Ibrahim Kirya ambaye mkataba wake wa ajira ulisitishwa na klabu.
Hii ilikuwa mara ya pili kwa
kocha huyo wa zamani wa Uganda Cranes kuifundisha watoza ushuru hao.
Mara ya kwanza, Nkata iliondoshwa
mara ya kwanza URA tarehe 18 Juni 2014 wakati huo CEO akiwa Dk. Jack Walugembe na
Alex Isabirye akawa kocha wa watoza ushuru hao.
Sam Ssimbwa huwenda
akaiongoza URA FC.
0 Comments:
Chapisha Maoni