Uongozi wa chama
cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam (BD) umethibitisha kupokea msaada wa
mabati na genereta kutoka kwa mkuu wa mkoa huo Paul Makonda, huku ukiweka
bayana kushindwa kuutumia msaada huo kutokana na sababu mbalimbali.
Hivi karibuni mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alishangazwa na BD kutoutumia msaada huo,
ili kuukarabati uwanja wa ndani wa taifa ambao ni chakavu kwa matumizi ya
michezo mbalimbali.
Mwenyekiti wa BD
Okare Omesu amesema wapo katika mchakato wa kuvutumia vifaa hivyo, japo
wanakabiliwa na fedha ya kufanikisha lengo hilo.
Pamoja na maelezo
hayo ya mwenyekiti wa BD, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameendelea
kushangazwa na hatua ya uongozi wa chama cha mpira wa kikapu mkoa huo kushindwa
kuutumia kwa vitendo msaada aliowapatia mwaka 2017.
0 Comments:
Chapisha Maoni