Tuzo ya
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajiwakufanyika Juni 23
mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kufanyika kwa tuzo
hizo ni utaratibu ambao Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), limejiwekea
kila mwaka baada ya kumalizika ligi kutoa tuzo kwa waliofanya vizuri kwa
kushirikiana na Wadhamini wakuu wa VPL Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom
Plc na msimu huu tutakuwa na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier
Bet.
Kaimu afisa habari
wa shirikisho la soka nchini TFF Clifford Mario Ndimbo, amesema licha ya Tuzo
ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, pia kunatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa
mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika
kuboresha.
Wakati huo huo Kamati
ya Tuzo za VPL, imekamilisha orodha ya awali ya wachezaji 30 kwa ajili ya
kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/18, ambayo sherehe
zake zitafanyika Juni 23 mwaka huu.
Kila mwezi Kamati
ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika
kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika
viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.
Wachezaji
walioshinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu na miezi yao katika mabano
nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq
Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
Wengine
ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC
ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John
Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji
wa Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza
(Aprili).
Wachezaji hao kila
mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil.
Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.
Hivyo wakati huu
tukielekea mwisho wa ligi, leo tunatangaza wachezaji 30 ambao watawania tuzo
hiyo, ambao watachujwa na kubaki 10, kisha watabaki watatu ambao ndiyo
wataingia fainali ya kuwania tuzo siku ya mwisho.
Wachezaji hao 30
ni Habibu Kyombo (Mbao), Khamis Mcha (RuvuShooting), Yahya Zayd, Razack
Abalora, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Himid Mao (Azam FC) Awesu
Awesu (Mwadui), Adam Salamba (Lipuli), Mohammed Rashid (Prisons), Shafiq
Batambuze, Mudathir Yahya (Singida United), Marcel Kaheza (Majimaji), Ditram
Nchimbi (Njombe Mji) Eliud Ambokile (Mbeya City), Tafadzwa Kutinyu (Singida
Utd), Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani (Young
Africans), Obrey Chirwa (Yanga), Aishi Manula, Emmanuel Okwi, John Bocco, Jonas
Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Asante Kwasi (Simba), Shaaban Nditi na
Hassan Dilunga (Mtibwa.)
0 Comments:
Chapisha Maoni