Jamii wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imetajwa
kuwa imekuwa mstari wa mbele kupata
huduma ya Tohara kwa wanaume.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya FootPrint, Dk.
Telence Mwakaliku wakati Akizungumza
na Huheso Fm.
Amesema kwa kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiendesha zoezi hilo Wilayani Kahama
kwenye halimashauri ya mji wa Kahama na Msalala jamii inaendelea kujitokeza kwa wingi katika
zoezi hilo.
Aidha mtoa huduma ya Tohara kwa wanaume kutika kituo cha Bakwata Nyahanga Bw.
Innocent Mtasingwa, amesema changamoto iliyobaki kwa sasa ni baadhi wa watoto kufika katika vituo vya
kutolea huduma bila kuwa na wazazi.
Kwa upande wake Tuombe Sylavanus
ambaye amepewa huduma ya Tohara kwa wanaume, amewahimiza vijana kujitokeza
kuendelea kujitokeza katika vituo vya afya.
Asasi ya FootPrint inajihusisha
na uhamasishaji wa mabadiliko ya tabia chanya na matumizi sahihi ya bidhaa
pamoja na huduma za afya, inatekeleza utoaji wa huduma ya tohara tangu Mei 14
na linatarajia kumalizika Juni 9 katika vituo 10 kwenye halimashauri ya msalala
na Kahama mji.
0 Comments:
Chapisha Maoni