Shirikisho la riadha duniani IAAF limeichagua Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya riadha ya dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20, itakayofanyika mwaka 2020.
Rais wa IAAF Sabastian Coe, ametangaza hatua
hiyo baada ya mkutano Mkuu wa Baraza la mchezo huo uliofanyika siku ya Ijumaa
jijini Buenos Aires nchini Argentina.
Jiji la Nairobi limepata fursa nyingine ya
kuandaa mashindano makubwa duniani baada ya mwaka 2017 kufanikisha wenyeji wa
mashindano ya dunia kwa vijana wasiozidi miaka 18.
Mashindano hayo yatafanyika katika uwanja wa
Kimataifa wa Michezo wa Kasarani jijini Nairobi.
Mashabiki 60,000 wanatarajiwa kushuhudia
mashindano hayo kama ilivyokuwa mwaka 2017.
Katibu katika Wizara ya Michezo nchini humo
Kirimi Kaberia amesema Kenya ni nyumbani kwa mchezo wa riadha na muhimu kwa
maisha ya wananchi wa taifa hilo.
Rais Uhuru Kenyatta amefurahia uamuzi wa
IAAF na kupitia ukurasa wake wa Twitter ameikaribisha dunia nchini Kenya mwaka
2020.
Mashindano hayo
yamepangwa kufanyika kati ya Julai tarehe 7-12.
0 Comments:
Chapisha Maoni